Ronaldo Akana Kumsaliti Mchumba Wake

Mrembo Anayedai Kula Uroda Na Ronaldo
Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba alichokuwa anakifanya ni mahojiano, na si kuwa na muda mtamu na modo wa Brazil kama ambavyo mrembo huyo alitangaza.
 
Hii ni mara baada ya habari zilizoandikwa na gazeti la Sun la Nchini Uingereza kwamba amemsaliti mchumba wake Irina Shayk masaa 48 kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Hayo yamekuja mara baada ya mrembo huyo mwenye miaka 27 Andressa Urach, maarufu kama Miss BumBum, kubainisha kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikula uroda naye.

Ronaldo amesema kwenye ukurasa wake wa twitter ‘kuna mtu anajitafutia umaarufu kwa kupitia akaunti yangu’.

Aliendelea kwa kusema: ‘Na nashangaa kwa nini hii inatokea siku moja kabla ya mechi muhimu kwa timu yangu. Hakika ni kitu ambacho kama kimepangwa ili kuvuruga maisha yangu binafsi.’
Ronaldo Na Demu Wake
Kauli zake zimekuja baada ya Urach, kudai kwamba mchezaji huyo alimualika chumbani kwake na kumlipa kiasi cha paundi 2,500 kwenye hoteli ya Villa Magna, kabla ya pambano la Ligi ya Mpira wa miguu kati ya Real na timu toka Ujerumani ya Borussia Dortmund.

Ila Ronaldo anasema kwamba hakuwa kumsaliti mchumba wake ambaye wapo kwenye mahusiano kwa miaka mitatu sasa.

Ronaldo  alimalizia kwa kuandika kwenye akaunti yake ya twitter: ‘Nataka kutanabaisha ni kweli kwamba nilikuwa kwenye hoteli ya Villa Magna siku ya April 22, kwa lengo la kufanya mahojiano na Manu Sainz, kitu ambacho muandishi huyo anaweza kukielezea. Mambo mengine yote yanayosemwa ni ya kubuni na sio halisi.’

No comments:

Post a Comment