Dadaz Nite Full Charge

Ni Mcharuko wa DADAZ  Nite ndani ya Galapo Club Masai Ilala,
Huku ukirudi ukiwa na Full Charge..!
Chini ya MILAZO one TWO ikianzia IJUMAA hii na kila IJUMAA..!
Kutakuwa na SHINDANO la wa'DADAz toka kitaa..!
Disco na GUEST Dj Mickie Love, Dan Chibo & Dj Fax..!
Kiingilio: Dadaz ni FREE & Kakaz ni bk 4 tu..!

Na kuanzia Jumapili hii na kila Jumapili MILAZO One TWO Inatambulisha kwenu JUMAPILI ya WABISHI wa TOWN..!
Je wewe ni MBISHI, KIBISHIBISHI ungana WENZA, huku ukipata ngoma kali sambamba na SHOW toka kwa WASANII..!
Kiingilio: Wanaume watalipa bk3 na wakipata KUPONI ya BIA MOJA ndani,
Wanawake wataingia bure, Karibu.

Inaletwa kwenu na MILAZO one two..!

read more "Dadaz Nite Full Charge"

Goldie Wa Big Brother Kuja Bongo

Prezzo & Goldie
Goldie ambae alikua mwakilishi wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa 2012 amethibitisha kwamba anakuja Tanzania mwanzoni mwa September 2012 kwa ajili ya kazi moja tu.
Goldie anakuja kwa ajili ya kutimiza lengo lake la kuingia studio na kurekodi kolabo na Ambene Yesaya a.k.a AY tu.
Amesema anafurahi kujua anakuja Tanzania ambapo tayari Ay ameshamuahidi kumpeleka na kumuonyesha sehemu mbalimbali za Tanzania.
AY
Goldie ambae ali-fall inlove kwa Prezzo wa Kenya alimfahamu Ay kwa Prezzo ambae alikua anamuongelea sana, pia kupitia nyimbo zake zilizokua zikipigwa kwenye jumba la Big Brother na hasa wakati alipokua akigombana na Prezzo.. Big Brother alikua anapiga single ya Ay na Sauti Sol wa Kenya ya I dont wanna walk alone.
read more "Goldie Wa Big Brother Kuja Bongo"

Msanii Keko Wa Uganda Amekuwa Chizi?Keko

Keko

Mitandao mingi ya kijamii imeejaa habari za rapa wa kike kutoka Uganda zikisema kwa amekuwa chizi, na hiini baada ya kuonekana akimkimbiza kibaka wa laptop.
Mitandao hiyo ya kijamii pia imeeleza kwamba Star huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter jinsi gani Uganda imekuwa si sehemu salama kwake na kuna watu wanahatarisha maisha yake, watu ambao walitaka kufahamu zaidi kuhusu stori hiyo, walijaribu kumpigia simu lakini matokeo yake ilipokelewa na dereva wa boda boda na hata alichokiongea kilionekana kutokuleta maaa yoyote.
Kitendo hicho cha Keko, kimewalazimu baadhi ya watu kuhitimisha kuwa amechizika, habari za hivi karibuni zinadai kuwa uchizi wa stori ya Keko ulikuwa ni stunt tu, aliyoitumia kufanya utafiti kujua ni kiasi gani anajulikana na watu
Keko ambae sasa yuko chini ya Sony Music Entertainment ameahirisha uzinduzi wa album yake mara tatu sasa ambapo alitangaza kuizindua mwezi wa nne tarehe 17 mpaka mwezi wa tano tarehe 4 na sasa kuipeleka mpaka mwezi wa nane tarehe 10, na inasemekana Sony nao wanataraji kutangaza siku yao ya kuzindua album hiyo.
read more "Msanii Keko Wa Uganda Amekuwa Chizi?Keko"

Man to Watch

Mbwana Samatta
Ilikuwa ni dakika ya 44 krosi toka kwa Trésor Mputu inatua kichwani kwa MBWANA SAMATTA na kuandika bao la pili, full time Zamalek 1 v TP Mazembe 2
Nyota wa Tanzania, Mbwana Ally Samata, jana alipiga Bao la pili na la ushindi kwa Timu yake TP Mazembe iliyoifunga Al Zamalek bao 2-1 katika Mechi ya klabu bingwa barani Afrika iliyochezwa huko Cairo, Misri bila ya Watazamaji wowote kufuatia kuzuiwa kwao kuingia kwenye Mechi baada ya Vifo Uwanjani kutokana vurugu mapema Mwaka huu.
TP Mazembe ya Congo DR ilitangulia kupata bao katika Dakika ya 34 lililofungwa na Hichani Homoonde na Al Zamalek wakasawazisha Dakika moja baadae kwa bao la Razak Omotoyossi.
Al Ahly ya Misri walitoka sare bao 1-1 huko Ghana na Bechem Chelsea lakini bado wanaongoza Kundi B wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na TP Mazembe.
Katika michuano ya kombe la shirikisho, timu iliyoitoa Simba ya Tanzania  Al Ahli Shandi kutoka Sudan ilipata ushindi ugenini wa bao 1 – 0 dhidi ya GD Interclube ya Angola.
 
read more "Man to Watch"

Top 10 Music Video za Kinigeria Zinazoongoza kutazamwa zaidi kwenye Youtube

P-Square
1. P-Square - Do
 Me 8,190,758 views

2. P-Square ft. Akon & May D - Chop My Money
 7,858,903 views

3. D'Banj - Oliver Twist
 5,035,658 views

4. Flavour - Nwa Baby (Ashawo Remix) Video
 4,457,160 views

5. P-Square - Beautiful Onyinye ft. Rick Ross [Official Video]
 3, 729, 635 views

6. P Square Ft J. Martins E No Easy (Official Video)
 2,912,350 views

7. Flavour - Oyi Remix ft. Tiwa Savage [Video]
 2,231,915 views

8. 5.Bracket - Girl Ft. Wizkid 3,208,276 views

9. VConnect Fever Video 2,018,238 views

10. P-Square - Forever
 1,906,905 views
read more "Top 10 Music Video za Kinigeria Zinazoongoza kutazamwa zaidi kwenye Youtube"

Q&A na Aunty Lulu: Aliyefungashia

Pozi tofauti
Q&A
 
AMEPATAJE MAKALIO HAYO?
“Makalio yangu nimeyarithi kutoka kwa mama yangu mzazi, japokuwa nikiwa mdogo nilikuwa mwembamba lakini nilivyokuwa mtu mzima ndiyo limekuja lenyewe hivi kama unavyoliona.”
USUMBUFU ANAOKUTANA NAO
“Napata usumbufu mkubwa sana, kila ninakopita wanaume wananiita pia nimekuwa nikipata mialiko mingi sana kutoka kwa wanaume wa sehemu  mbalimbali ambao hata siwafahamu.”
 
Kwenye pozi Kitandani
 JE, ANATAMANI KUPUNGUA?
“Weeee……thubutu! Sitamani hata kidogo kupungua kwa sababu makalio yangu nayapenda sana, pia yananipa faraja kubwa yaani Mungu amenipendelea.”
KUHUSU MAVAZI YAKE
“Napenda kuvaa nguo zinazoachia mwili wangu kama gauni, huwa najisikia niko huru zaidi.
SAIZI YA NGUO YA NDANI
“Sijui saizi ninayovaa maana sivaagi kufuli kwa sababu nikivaa huwa najikuna sana kutokana na hali ya joto.”

CHANZO: Global Publishers
read more "Q&A na Aunty Lulu: Aliyefungashia"

Koffi afikishwa kwa Pilato

Koffi Olomide
Mwanamuzi mashuhuri nchini kongo(DRC) Anton Akgeba Makila Mabe maarufu pia kama Koffi Olomide aka Mopao Mokonzi, Aswekwa lupango na pia kafikishwa kwa Pilato
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.

read more "Koffi afikishwa kwa Pilato"

Ndoa ya Uwoya yasukwa tena

Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’
 NDOA ya staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ina dalili za kurejea kwenye hali ya amani baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa, kuna vikao vinafanyika kwa lengo la kuihuisha.
Chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake ambacho ni mmoja kati ya marafiki wa Irene kililitonya Ijumaa kuwa, yeye na watu wengine wa karibu wa msanii huyo wamedhamiria kuwarudisha wawili hao kwenye furaha kwani wanaamini bado wanapendana.
“Tunachokifanya sasa tunakutana mara kwa mara kuangalia kama tunaweza kutumia mbinu gani kuhakikisha ndoa ya Uwoya na Ndikumana inatengemaa. Kwa kifupi tunaisuka upya,” alidai sosi huyo na kuongeza:
“Unajua kwa watu unaowapenda huwezi kufurahi kuwaona wakiwa mbali, sisi tunaamini tutafanikiwa katika hili, tunajua Irene anampenda Ndiku na Ndiku anampenda Irene ‘so’ ni lazima kieleweke.
Baada ya kunyetishiwa habari hiyo, Ijumaa lilimtafuta Irene ili kujua kama anajua lolote kuhusiana na vikao hivyo lakini hakuweza kupatikana.
Hata hivyo, Ndikumana aliwahi kuongea na moja ya magazeti ya Global Publishers na kusema kuwa hajavunja ndoa na Irene hivyo inaaminika siku yoyote mambo yatakuwa freshi.
read more "Ndoa ya Uwoya yasukwa tena"

Tyga aja na Single Mpya

Tyga

Msanii wa Young Money mkali wa ngoma ya “Rock City” Tyga anaachia ngoma inaitwa “Diced Pineapples”  ikiwa ni remix amechukua mistari ya ngoma ya God Forgive, I don’t cut ya Rick Ross akafanya ngoma hiyo kwa ajili ya mixtape yake inayoitwa Well Done 3 ambayo inatoka Jumapili hii usiku saa 6. 
read more "Tyga aja na Single Mpya"